Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini Izzo Bizness akiwapagawisha washabiki
katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa
Lake Tanganyika mjini Kigoma
Umati
wa mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha la Kili Music Tour,
wakifuatilia onyesho hilo lililofanyioka kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika, Kigoma.
Baadhi
ya wasanii wa muziki nchini wakiwa pamoja na Meneja wa bia ya
Kilimanjaro, George Kavishe katika tamasha la Kili Music Tour
lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ akifanya yake
katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika Kigoma.
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Joseph Haule ‘Profesa Jay’ akitumbuiza katika tamasha la Kili Music Tour Kigoma.
Diamond
akiongoza wasanii wenzake Mwasiti, Linex na Recho katika nyimbo ya
‘Leka Dutigite’ na kuwaamsha mashabiki waliofurika uwanja wa Lake
Tanganyika katika tamasha la Kili Music Tour, mjini Kigoma.
Msanii
wa muziki nchini Lady Jaydee ‘Jide’ akitumbuiza kwenye tamasha la Kili
Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wLake Tanganyika mjini Kigoma.
Na Mwandishi Wetu
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul, juzi alifunika katika
tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika Mjini Kigoma.
Katika
tamasha hilo lililohudhuriwa na umati wa mashabiki, Diamond alifanya
onyesho la aina yake na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa kupiga
kelele.
Diamond ambaye alikuwa msanii wa mwisho kupanda kwenye
jukwaa, aliwaita wasanii wenzake ambao ndio wenyeji wa Kigoma kama
Recho, Mwasiti pamoja na Linex na kuimba wimbo wa Leka Dutigite na
kuwaamsha mashabiki waliofurika Uwanjani hapo.
Wasanii
wengine ambao walitumbuiza katika onyesho hilo lenye ujumbe wa ‘Kikwetu
Kwetu’ ilikuwa ni pamoja na Lady Jaydee, Barnaba, Ben Pol, Izzo
Bizness, Recho, Prof. J, Fid. Q, Roma, Mwasiti, Linex pamoja na Kala
Jeremiah.
No comments:
Post a Comment